Na.
Dezidery Kajuna
Vijana
tunaweza kuleta mabadiliko, tukiwezeshwa na kupewa nafasi katika nyanja mabali
mbali. Pia tunaweza kuleta maendeleo endapo jamii itatuthamini na kutukabidhi
madaraka. Tatizo wengi wetu tumeshindwa kujitambua kuwa -tunaweza na
tunavipaji.
Kuna
mitazamo mingi juu ya “ ujana”, “kijana”., Ukiacha tafsri zinazogusa
umri(ambazo zinatofautiana baina ya nchi na nchi), zaid kijana anapaswa hasa
kuwa na sifa zikiwemo; fikra mpya na uwezo
wa haraka wa kuibua mawazo mapya. Wengine wanaita ujana ni damu change
inayochemka!
Kijana
pia upambanaji wake ni wa kiujana zaidi.
Haijalishi ni mapambano ya aina gani. Ukumbuke
kuna mapambano ya kimaisha yaani mtu binafsi, kisiasa, kijamii, kwa ujumla kupambana
kwa ajili ya jamii inayokuzunguka.
Neno uongozi
si neno jipya na wala si geni masikioni hata machoni petu ni kimaanisha
tunawajua viongozi na tunaweza kuwaona na kuwagawa katika makundi kutokana na
uongozi wao na mafanikio yao. Ila
tukumbuke uongozi upo katika makundi ya kwamba kuna ule uongozi wa kimabavu au
kiimla na ule uongozi usio kuwa wa kimabavu, unaofuata sheria na katiba
zilizowekwa kwa makubaliano katika kikundi, jamii au nchi fulani.
Kuna kitabu
kinaitwa “Uongozi bora” kilichoandikwa na Mahnaz Afkhami,Ann Eisenberg na Haleh Vaziri kwa
msaada wa Suheir AzzouniAyesha Imam, Amina Lemrini, Rabéa
Naciri -wanasema “Uongozi ni uwezo wa kubuni na kuyaweka maono katika vitendo”. Japo kuna
vitabu vingi vilivyo andika juu tafsri ya neno uongozi . Hivyo
basi suala la uongozi ni muhimu kwa kila
mtu.
Kwa mtazamo huu haijalishi wewe ni mzee kwa maana ya kwamba una zaidi ya miaka 40 au upo chini ya miaka 18. Kama wewe ni
mzee basi kumbuka unahusika maana wewe ni tunu na ni muhimu katika kumjenga
kijana ili awe bora katika siku za usoni. Kama wewe upo chini ya miaka 18 basi
kumbuka una fursa ya kujifunza na kujiandaa kuwa kiongozi bora siku za usoni.
Tanzania
ni nchi moja wapo iliyobarikiwa kuwa na watu, si maanishi kuwa nchi ikiwa na
watu wachache imelaaniwa- , la hasha! Hapana, dhana yangu inabebwa na imani
kuwa mkiwa wengi ni rahisi kulifanya jambo gumu kuwa jepesi kwa dhana ya
kusaidiana, ujuzi kuwa mwingi kwa idadi ya watu, uzalishaji kuwa mkubwa maana
utendaji- wa ndani unakuwa mkubwa.
Jambo muhimu
kulielewa ni nani anapaswa kuwa kiongozi na nani hapaswi kuwa kiongozi. Wewe
kama ni kijana na unataka au unahisi una talanta ya uongozi basi huna budi kuanza
kujifunza juu ya uongozi. Kuna njia au nafasi nyingi za kuweza kujiandaa kuwa
kiongozi, unaweza shiriki katika mafunzo ya uongozi, warsha za uongozi, mikutano
na makongamano yanayo husu uongozi au kujituma pale unapopewa majukumu ya
kawaida.
Mfano unaweza kuchukua nafasi ya uongozi nyumbani kwa kuhakikisha
watu wanafanya kazi kwa misingi ya kugawana kazi, mtaani au kijijini kwenu unaweza pia kushiriki kutoa mawazo
ambayo unadhani yatasadia kuleta amani, uwajibikaji, utendaji madhubuti, kwa mfano ulipaji wa pesa za taka, usafishaji
wa mitaa au vijiji, lakini pia unaweza chukua jukumu la kuongoza watoto hapo
mtaani au kijijini, kwa mfano juu ya tabia njema, kuheshimu wazazi, kuwa na
upendo katika jamii husika, kusoma kwa bidii, na wao watatambua na kukumbuka
kwa mchango wako na hapo ndipo utakapo jifunza ni maana ya uongozi.
Uongozi
ni kukubali majukumu na kuyasimamia kwa umakini, utashi, ukarimu, usitaarabu au
busara, uwajibikaji, ukweli na uwazi, usawa bila kujali itikadi za kidini,
kirangi, kabila au ukanda. Si rahisi sana kuwa na vitu hivi vyote inahitaji
moyo, kujituma na kujifunza kutoka kwa watu walio kutangulia, watu unao ongoza
na jamii husika inayokuzunguka.
Ikumbukwe
kuwa pia kiongozi ni mtu anayeheshimu wa watu wa rika zote bila kujali kiwango
cha uelewa wao, umri, elimu yao, na kiasi cha mali walizo nazo. Kiongozi ujifunza
kila sekunde,dakika, saa, siku,-wiki, mwezi na hatimaye mwaka. Namaanisha kiongozi
ni yule ajifanyaye mjinga kiasi cha kutaka kujua jambo kila siku iendayo kwa
Mwenyezi Mungu.
Kama
unataka kuwa kiongozi ila una ugonjwa wa kutopenda kuerekebishwa au kuwajibishwa
basi jifunze kujishusha. Kujishusha ni siraha kubwa sana kwa mtu anayehitaji
kuwa kiongozi bora katika jamii. ‘
Kijana
kiongozi, ni mtu anayetegemewa kuwa hana makuu, si mpenda ugomvi, si mlevi
kupindukia kiasi cha kuleta kizaazaa kwa jamii husika, si mtu mwenye kashfa
maana vijana wengine na hata watu wazima watajifunza mema na mabaya kutoka
kwako. Hivyo kiongozi kijana ni yule atakaye epuka haya yote.
Kwa
sasa Tanzania, ni moja ya nchi chache duniani ambazo vijana wake wana hari
kubwa katika masuala ya uongozi haswa kisiasa. Ila safari bado ni ndefu maana,
uwajibikaji, uwazi na na utendaji madhubuti ni tatizo kubwa kwa jamii nzima, na
kwa serikali kiujumla.
Vijana
wa sasa, hapa Tanzania hatuna darasa la uongozi mathalani -serikalini, kwani serikalini hatujaona mtu wa kuiga au mfano
bora katika uongozi, ni majungu, ukabila, ukanda, undugu, rushwa, na ushirikina.
-Naomba nieleweke vizuri hapa majungu na-maanisiha watu wamekaa kusemana,
kupigana vita na hata kuchongeana maneno yasiyo na tija, ukabila hilo
linajulikana sana kwa jinsi viongozi na makabila yao wanavyojineemesha kwa
kupeana nafasi za uongozi.
Undugu,
hili si geni, tunajua jinsi ambavyo watu walivyojazana katika maofisi kwa mgao
wa kikabila, mtu anapewa kazi au uongozi kwa misingi ya ukabila Rushwa, hii
imekuwa kama wimbo, mtu yupo radhi kuitoa roho ya mwenzake kisa amekataa
kupokea rushwa, tena rushwa imekwenda mbali zaidi imeingia mpaka katika taasisi
nyeti kama mahakama, polisi na hosipitalini na makanisani je ni nani atapona
kwa hili?
Ushirikina, kwa hili naomba tuelewe kuwa
mchawi ni mchawi na mshirikina ni mshirikina haimaniishi unatoka wapi na kabila
gani. Ushirikina kwa sasa unatumika kama chombo cha kujikomboa katika uongozi,
zamani watu walikuwa wanaomba ruhusa za kwenda kusoma ili kujiongezea elimu kwa
maana ya ujuzi ila kwa sasa watu wanaomba ruhusa za kwenda kwa waganga mwishowe
taifa linaangamia kwa sababu watu wamekosa maarifa.
Vijana,
nawaomba tujifunze kutoka katika hayo niliyoyaeleza, tukumbuke kiongozi
hafufuki au haji kwa njia za undugu, ukabila, ukanda au ushirikina. Kiongozi
anaandaliwa na kwa kutambua wito uliondani yake mwenyewe. Kiongozi anajifunza
kutoka kwa wengine, kiongozi anaenda darasani kusomea ujuzi.
Na
uongozi ni wito, si eti kwa sababu baba ni waziri au mbunge basin a wewe
unaweza kuwa kiongozi la hasha, kama ni wito utakuwa kiongozi. Ila cha msingi
uongozi ni mafunzo ndo maana wenzetu wa nchi zilizoendelea wanaamini mtu aliye
na ujuzi na aliyeusomea na kuishi kwa muda ndie kiongozi bora. Vijana amkeni,
wakati ndo huu, fursa ni yenu kujifunza, kujitoa kwa ajili ya nchi yetu,
kupambana na ujinga, rushwa, ushirikina, kuwajibika kwa uhakika, kuwa wazi,
kuwa watendaji wa kweli na kujifunza kutoka kwa walio na mafanikio katika
uongozi.
Kiongozi
bora hategemei ushabiki wa vyama, ila
anajifunza na kutenda kadri ya sheria za nchi. Kijana aliye na nafasi kuwa
kiongozi ni Yule anayetambua kuwa hakuna binadamu aliye juu ya sheria, hakuna
aliyekamilika kimaadili, kimawazo, kiutendaji na hivyo kila mtu ana mapungufu. Tuchague kilicho bora kwa kwa misingi ya kuleta
maandeleo. Kama ni kuchagua basi wewe kijana chagua mtu aliye na sifa nilizo zilizotajwa
hapo juu, usichague mtu kwa sababu ni mhaya, msukuma, mchaga, mpare, au eti ni
kabila lako, hapana usifanye hivyo!
Pia
tusichague mtu eti kisa ana pesa au umepokea pesa kutoka kwakwe. Jifunze kusema
hapana kwa ufedhuli wa namna hiyo, jifunze kuchagua kilicho bora, jifunze
kuipenda nchi yako na watu wako.
Jambo
muhimu la kukumbuka ni kwamba kiongozi bora na kijana mdadisi ni yule asiye
penda sifa au kusifiwa vijana wa kileo wanawaita -”mpenda masifa”- na ambaye atakuwa tayari kukosolewa na kujierekebisha.
Kiongozi ni yule mwenye siko pana namaannisha aliyetayari kusikiliza watu na
mahitaji yao.
Nakumbuka
kuwa niliwahi kugundua kuwa hata wanaoongozwa wanaweza kuwa sehemu ya darasa
kwa viongozi. Wale wanaoongozwa si bubu na wala si wajinga ni watu wenye akili
timamu na chanya na wana michago mingi sana juu ya kipi kifanyike na kipi
kisifanyike. Tujifunze kusikiliza watu tunaoongoza katika nyanja mbali
mbali. Kuna mifano mingi ambayo tunaweza
kujifunzia kutoka kwa watu mashuhuri
waliowahi kuwepo na waliopo hapa duniani kwa sasa.
Lakini kihisitoria tunajifunza na kupata kujua kuwa
Mwana falsafa maharufu kama Plato katika
maandishi yake aliwahi kusema “ Leaders must understand that
their daily choices, judgment calls, behaviors and actions matter and make a
difference–they have meaning. Leaders are called to the higher realm of
intelligence and accountability and must help others, (akimaanisha kuwa
, Viongozi lazima waelewe ya kuwa maamuzi, tabia na matendo yao ya kila
siku ni muhimu na yana maana. Viongozi wamepewa uwezo mkubwa wa kiakili na
kiuwajibikaji na inawapasa kusaidia wengine)
Ni kama
vile kauli ambayo akipata kuitoa Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mheshimiwa Freeman
Mbow akisema kuwa viongozi wanatengenezwa. Ni kweli! Lakini pia hata taifa madhubuti na lenye mafanikio
utengenezwa pia tukirudi kwa Plato aliwahi kusema -” therefore we need not to expect to have
better states until we have better men” (akimaanisha,-hivyo basi hatuitaji ku-tegemea kuwa na taifa bora mpaka tupate watu
bora-akimaanisha viongozi bora).
Huo
ndio kweli, kuwa taifa halijengwi na vijana au watu legelege, wala rushwa, watu
wa kuchaguana kiukanda au kikabila bali taifa hujengwa na watu bora yaani
viongozi bora. Tuache kulalamika, tukae chini na kasha tutafakari ni kwa jinsi
gani tutaweza kujenga viongozi bora kwa sasa na baadae. Wahenga walipata kunena
“Usione vyaelea vimeundwa”
No comments:
Post a Comment