Na Dezidery .K
Nalazimika
kuandika makala hii ili kuhamasisha mabadiliko katika sekta ya afya.
Kwanza kabla ya yote ifahamike kuwa mabadiliko yoyote yale na popote
pale si jukumu la serikali peke yake bali ni jukumu la wananchi
katika jamii yoyote inayotaka maendeleo ya kweli.
Tanzania
ni mmoja ya nchi masikini zinazo endelea kushuhudia matukio ya
kusikitisha sana katika utoaji wa huduma za afya. Utoaji huu wa huduma
za afya kwa asilimia kubwa ni ule usiofuata taratibu na kanuni za
utabibu. Inawezekana tumepoteza ndugu wengi kwa uzembe wa manesi na
madaktari wasio zingatia taaluma zao.
Katika
hili jamii imekuwa ni- ya kubeba, kuzika na kuombeleza vifo vya ndugu
zetu bila kuhoji walakini wa huduma walizo pewa ndugu zetu. Inawezekana
ni uelewa mdogo wa watu katika kuhoji haki zao na pia inawezekana ni
umakini mdogo wa wataalamu wa afya katika vituo vya afya.
Ni
ukweli usipingika kuwa hakuna anaye penda kufa lakini kwa kuwa kifo ni
sehemu ya maisha ya mwanadamu basi siku ikifika hatutakuwa na namna.
Lakini si vifo vyote ufuata mpango huo wa maisha ya mwanadamu. Vifo
vingine ni matokeo ya uzembe wa aidha upande wa mwadhirika au mtoaji
huduma. Hata hivyo tumekuwa tunasingizia Mungu sana, yaani kila msiba ni
mpango wa Mungu.
Misiba
hii imekuwa ikinakishiwa na maneno kama vile "Ni Mpango wa Mungu".
Lakini swali ni Je ni nani mwenye udhibitisho kuwa kifo au vifo hivyo
vilikuwa ni matoke ya mpango wa Mungu? Ni swali gumu lisilo na jibu
maana lazima jamii ikubali kuwa kuna uzembe mkubwa unfanyika katika
vituo vya afya zetu.
Kuna matukio mengi yaliyotokea ambayo ni ishara kuwa kuna uwalakini katika huduma za afya zinzotolewa katika hosipitali zetu. Moja ya tukio ninalolijua vizuri na pengine kunihuzunisha sana ni kifo cha ndugu yangu. Tukio lilitokea mwaka 2010 mwezi tatu (Machi), ndugu yangu huyu alikuwa amepatwa na homa ya gafra na baada ya masaa machache alipata msaada wa rafiki zake kumpeleka hospitali ya wilaya ya Temeke (Temeke Hospital), alipofikishwa pale aliwekewa drip, yaani mara nyingi "drip" ndo inakuwaga ya kwanza kabla ya vipimo. Basi, kaka yangu huyu alilala hapo mpaka asubuhi nilipofika hapo akiwa bado na kopo la drip.
Nilipofika
pale nilienda moja kwa moja mpaka kwenye chumba cha manesi, niliulizia
habari ya ndugu yangu. Jibu lilikuwa na la mshangao sana, niliambiwa
huyu bwana kaja kaletwa hapa akiwa na homa sana na tulipo mcheki
tukagundua hana pesa mfukoni hivyo tuka msadia drip. Sasa jiulize drip
hiyo mmoja ili msaidia nini katika usiku wote ule pasipo vipimo?
Niliondoka
katika chumba hicho cha manenisi kwa mshangao wa majibu yao. Moja kwa
moja nilienda katika kitanda cha mgonjwa wangu, kutoka na hali mbaya
niliyo ikuta pale ilitubidi tumbadilishe mavazi yake kisha tumtafute
daktari, katika haraka hizo ndugu yetu alitutoka na ukawa ndo mwisho
wake wa maisha hapa duniani.
Ni
miaka zaidi ya mitano imepita sasa bado najiuliza Je angepata huduma
nzuri kwa muda ule wa jioni alipofikishwa pale si angekuwa hai? Au
majibu ya vipimo yangetoa mwangaza wa wapi apelekwa ili apate huduma
bora.
Ngoja
niishie hapo, hivi majuzi juzi tukio lingine limetokea huko Bunda.
Katibu msadizi wa CCM amepoteza maisha kwa staili ile ile. Najiuliza
hivi hawa manesi wameajiliwa na nani? Au ni mfumo mzima wa afya umekosa
muongozo. Hayo ni baadhi ya matukio machache tu, lakini tukiomba
kufanya utafiti na kuzunguka nchi nzima bila shaka tunaweza pata matukio
zaidi ya elfumoja ya namna hii.
Tunahitaji
mabadiliko makubwa sana katika huduma hizi. Katika jambo lisilohitaji
matabaka ni hili la huduma za afya. Kila mtu ana haki ya kupata huduma
za afya bila kujali kipato chake. Nchi inapoteza nguvu kazi kwa uzembe
wenye tiba. Serikali inabidi ichambue matatizo kiundani zaidi badala ya
kuyaangali kijujuuu tu.
Mabadiliko
ni safari na tena yenye mwisho. Mwisho wenyewe ni ufanisi wa utendaji
katika mfumo mzima. Palipo na lengo la kweli matokeo uonekana dhahiri.
Hivyo
hivyo, sekta ya afya inahitaji mabadiliko makubwa na tena yenye tija
bila kujali hudama hiyo inatolewa kwa mtu wa aina gani. Mabadiliko haya
yanahitaji malengo ya kweli kwa faida ya wananchi wote.
Mageuzi yasipo fanyika sote tutakuwa wahanga wa "Mpango wa Mungu"
No comments:
Post a Comment