Na. Dezidery Kajuna
Ni
mwaka sasa toka mapinduzi katika nchi za kiarabu yaanze. Ukweli ni kwamba dunia
imeona mengi hasa mwaka uliopita yaani 2011. Mapinduzi hayo yalileta
mkanganyiko kwa wengi hasa watalawa katika nchi nyingi barani Afrika na nchi
nyingine za kiarabu.
Tukumbuke,
mapinduzi yale yalianzia Tunisia kisha, Misri
na baada ya siku kadhaa Libya nao wakaanza mikakati ya mapinduzi
yaliyopelekea kiongozi wa muda mrefu katika taifa hilo Muammar Ghaddafi
kuuwawa. Wingu hilo la mapinduzi
halikuishia hapo bali liliendelea katika nchi nyingine kama vile Yemen, Bahrain
na kwa sasa Syria ambako vyombo vya kimataifa vinaharifu kuwa hali inazidi kuwa
tete, mamia ya watu wakiangamizana.
Mada
yangu leo si kuzungumzia juu ya
mapinduzi hayo bali ni kueleza adhari
ambazo zimejitokeza haswa kwa upande wa nchi za ulaya ambazo kwa njia moja au
nyingine ndizo zilizo chochea moto katika mataifa haya ninayozungumzia.
Tulishududia mataifa makubwa kama ufaransa, Marekani, na washirika wao wakipiga kelele na kulaani
utawala uliokuwa karibu na mataifa ninayo yataja kiurafiki katika Nyanja zote
kisiasa, kiuchumi na kisiasa.
Tukumbuke
pia ubabe na uwezo wa vyombo vya kivita jinsi vilivyotumika kuangamiza mamia ya
watu kwa misingi ya kutetea demokrasia.
Nina sema kuangamiza watu kwa
sababu naamini kuwa demokrasia si kuangamiza watu bali ni mazungumzo na
maelewano kati ya pande zinazo zozana.
Ukweli
utabaki kuwa pale pale kuwa mwaka 2011 haukuwa mwaka mwepesi au raisi kwa
mataifa mbali mbali. Japokuwa tuna la kujifunza kama watanzania. Na kumbuka
kipindi cha vuguvugu hili la mapinduzi huko Afrika kasikazini vuguvugu hilo
lilinukia pia hapa Tanzania. Chadema hawakuwa nyuma, nao walikuwa na lao katika
kupambana na utawala wa Mheshimiwa Jakaya Kikwete. Naomba nieleweke hapa, Chadema walikuwa
si tu wanapambana , bali walikuwa
wanatetea na kupigania haki za watanzania kuwa na maisha bora, katiba bora, kulikabili
anguko la uchumi. Nguvu za dola zilitumika sana japo hazikushinda nguvu ya
umma.
Uganda
pia nako kulikuwa na vuguvugu la aina yake , naweza kulifananisha vuguvugu lile
na hili la Tanzania. Japo kule nchini
Uganda Dk. Kizza Besigye na washirika wenzake hawakufanikiwa sana kama hapa
Tanzania hii inatokana na aina mfumo na mtandao wa wanachadema kuwa imara sana na kulinganisha na majirani zetu Uganda. Sitaki
kulizungumuzia hili ila kiufupi ni kwamba utawala wa Uganda ni wa kijeshi, kiundugu
mpaka hata kwenye taasisi nyeti kabisa na Rais hawezi kusalitiwa kwa maana hana
mtandao bali anaabudiwa na wote walio nae katika utawala wake kama sehemu ya
fadhira.
Nirudi
kwenye mada yangu, vuguvugu lile la mapinduzi limeleta baraa kubwa katika
barani Ulaya katika nchi nyingi haswa Ulaya mashariki na baadhi ya nchi ya ulaya
magharibi. Adhari hizi zinatokana na sera, mahusiano yaliyopo na nchi husika
zilipo kwenye machafuko, pia na nafasi ya nchi katika baraza la umoja wa
mataifa katika kusaidia wakimbizi. Na ikumbukwe pia machafuko haya yaliambatana na anguko la KIuchumi duniani mbalo bado lina
sumbua sana nchi nyingi duniani.
Kule
nchini Italia hali ilikuwa mbaya sana mbali na uchumi wa nchi hiyo kuwa mmbaya
wakimbizi walikuwa wengi sana wengi wao wakitumia njia ya bahari kwa kutumia
vyombo hatarishi. Italia ndio nchi pekee inayosemekana kuwa ilipokea wakimbizi
wengi kutoka Libya. Ifahamike kuwa nchi za ulaya huwatambua wakimbizi kama raia
wao, na pia upewa haki sawa kama raia wengine. Ongezeko hili la watu,
limepelekea kuwepo tatizo kubwa la ajira kwa raia walio wengi haswa vijana.
Maandamano yalikuwepo kila wakati na mwisho wa yote ili lazimika Waziri Mkuu
Silvio Berluscon kujiuzuru huku rais wan
chi hiyo Giorgio Napolitano akimteua Mario Monti kuwa Waziri Mkuu mpya sambamba
na kukabiliana na hali ya kichumi.
Hali
hii iliikumba pia nchi ya Ugiriki, watu wengi wanadhani hali ya kiuchumi tu
ndio imepelekea mataifa haya makubwa kukumbwa na misukosuko, la hasha! Ugiriki
ni nchi moja wapo isiyokuwa na sera na mikakati madhubuti ya kupambana na
ongezeko la wahamiaji. Na hili lilipelekea uchumi wa nchi hiyo kudorora mpaka
kupelekea waziri mkuu wan chi hiyo George Papandreou kujiuzuru. Huku waziri mpya Lucas Papademos
akiteuliwa lakini hali bado si nzuri.
Nchini Ufaransa Taifa kubwa kabisa lakini nalo nadhani linajutia sana
maamuzi yake ya kuingilia mambo ya Kisiasa kwani inaelezwa kuwa nayo ni nchi
mmoja wapo iliyopokea wahamiaji wengi, wengi wao wakitoka Tunisia, Ivory coast
na pia Libya. Ajira ni tatizo kubwa nchini Ufaransa kwani, kila kukicha kuna
ongezeko kubwa la wahamiaji na wengi wao hawana makazi na ajira ukilinganisha
nchi zingine kama Uingereza, Ujerumani, Sweden, Norway, Uholanzi, na Finland. Wizi kama ule wa kariakoo wa kukwapua mabegi
ya watu au simu unaripotiwa kuwa ni kama jambo la kawadia kwa sasa nchini
Ufaransa.
Nchini
Sweden, Norway na Finland madhara ya
wimbi la mabadiriko ya kisiasa Afrika magharibi na mashariki ya kati
zinaonekana haswa katika Nyanja ya ajira na si makazi. Ajira nyingi haswa kwa
wageni wanao zamia na wanaoenda kwa
ajili ya masomo imekuwa tabu sana. Hii inatokana na sera ya nchi hizi kuwathamini
sana wakimbizi hasa wale waliopokelewa na mamlaka husika kwa kuzingatia vigezo
vya shirika la kusaidia wakimbizi duniani.
Nchini Sweden, serikali inahusika moja kwa moja kuwatafutia kazi
wakimbizi, kuwapatia makazi, na pesa ya kujikimu kupitia almashauri za nchi hiyo. Hivyo imepelekea pia raia wengi kutoka barani
Afrika na sehemu zingine kukosa ajira hasa walio masomoni na wahamiaji haramu
(wasio tambuliwa). Naomba ifahamike kuwa
mkimbizi anayetoka katika nchi iliyo kwenye machafuko anathaminiwa sana na
kulindwa kuliko yule aliyetoka nchi zisizo kwenye machafuko kama Tanzania, Kenya, Uganda na nchi nyingine
nyingi.
Ongezeko
hili la watu limekuwa ni bomu jipya katika nchi hizi za ulaya, na hii
imepelekea kuanzishwa kwa mchakato wa kupunguza idadi ya wakimbizi, kutopokea
wakimbizi kwa maana ya kuwasaidia ndani ya mipaka ya nchi zao. Lakini pia hatua
zaidi zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na kulinda mipaka ya nchi, kwa kuanzisha mfumo jumuishi wa mkutambua mtu kwa kutumia vidole vya
mhusika balani ulaya kote .
Nacho maanisha hapa ni kwamba kwa sasa kila raia
awe ni mzaliwa wa hapo au muhamiaji wote watakuwa na vitambulisho vilivyo na
alama za vidole vyao zilizochukuliwa kwa mashine maalumu. Kwa hiyo kuvuka
mipika ya nchi mmoja kwenda nchi nyingine itakuwa kazi kweli kweli. Mfano mzuri ni Sweden ambao wao wamekwisha
anzisha mifumo yote hiyo pamoja na punguzo la kupokea wakimbizi kwa asimilia tisini na nane
kuanzia mwaka jana.
Kwetu
hapa Tanzani sidhani kama mambo haya yanawezekana kwa maana hatuna mifumo
dhabiti ya kukabiliana na wakimbizi, utawala haupo makini, rushwa inatumika sana
na uelewa wa waliopewa mamlaka ni mdogo sana.
Tunahitaji mapadiliko makubwa
katika chombo chenye dhamana husika. HIli nalo ni bomu ambalo linaweza kuongeza
adhari zaidi kwetu kwa maana ya kwamba tayari tumekwisha shuduhudia adhari hizo
ikiwa ni pamoja na waasia tunao waona hapa nchini ambao wengi wao wameingia
kinyemera kwa msaada wa rushwa. Ajira nyingi ndani ya viwanda vinavyo milikiwa
na wahindi , wapakistani na wachina zimechukuliwa na wageni huku wenyeji wakiwa
hawana pa kukimbilia. Tunahitaji mabadiliko katika jambo hili, na hatua muhimu
lazima zichukuliwe. Tunahitaji kusimamia raslimali zetu vizuri, mazingira bora
ya kazi kwa watanzania ni haki yetu na
ni wajibu wa serikali kuwa sera mbadala na mikakati madhubuti katika
kulisimamia jambo hili.
No comments:
Post a Comment