Friday 25 March 2016

"ULAYA HAKUNA MAISHA MAZURI"

Na. Dezidery Kajuna

"Ulaya kuna maisha mazuri" huu ni usemi maarufu sana barani Afrika na nchi nyingi za Amerika ya kusini na Kasikazini. Nakumbuka "enzi" fulani hivi wakati nasoma shule ya msingi, niliwahi kuwa mtu mzuri wa kuadithia watu juu ya jinsi ulaya kulivyo kuzuri. Tena nakumbuka jinsi nilivyokuwa naelezea maisha ya huko utadhani nimezawaliwa huko. Wenzangu wakidhani mimi nimetoka huko majuzi juzi tu, huku walinikodolea macho  mithili ya "watoto" wa uswahilini watazamao filamu ya "Rambo" iliyo tafsiriwa katika lugha ya kiswahili.

Laiti, wangelijua kuwa sikuwahi kufika huko na wala sikuwa na ndugu aliyekuwa huko wakati huo, wasinge poteza muda wao, wa kusikiliza habari isiyo ya kweli, ilikuwa ni akili ya kitoto iliyo sukumwa na filamu za ulaya zikionesha mandhari yake.  Naam, miaka ishirini na sita baadae nikapata bahati ya kwenda huko Ulaya ambako niliamini ni kuzuri na ndiko dunia halisi iliko. Amini usiamini mababu zetu waliwahi kunena "Usilo lijua ni kama usiku wa giza" Ni kweli sikulijua giza lilipo huko Ulaya.

Sikujua hadithi zile kwa wanafunzi wenzangu, zilikuwa ni ndoto za uongo, yalikuwa ni maneno ya kupotezeana muda, nilikuwa nawalisha wenzangu viazi vibichi. Hatimaye miaka ikaenda nikapata nafasi ya kwenda huko. Ngoja niliseme hili, hivi mwajua kuwa watu wengi waendao ulaya  hawaelezi ukweli halisi wa jinsi hiyo ulaya ilivyo? Wengi wao wanaelezea mazuri tu, wachache sana watakueleza mabaya yaliyo jificha.


Jamani "Ulaya hakuna maisha Mazuri" hili ndilo lengo langu kuu la kuandika mada hii. Tena kikubwa kilicho nisukuma ni ongezeko la vifo vya wahaamiji huko katika bahari ya Mediterranian wakielekea Italia iliyoko balani Ulaya.  Hali hii ilianza kama 'mzaa', na sasa imekuwa 'usaa' Wahamiaji hawa wengi wao wanatoka Ethiopia, Eritrea, Sudan, Somali, Senegar, Mali, Nigeria, Cameroon, Gambia na Ghana. Hatuwezi fahamu, pengine wapo wa kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Congo DRC na Burundi.

Inasemekakana kuwa vifo vya wahamiaji hawa sasa vimeongezekama mara therathini zaidi ya vile vile tokea katika kipindi cha mwaka 2014. Ikumbukwe kuwa mwaka 2013 vifo vya wahamiaji katika bahari ya mediterrania vilikuwa ni zaidi ya watu 300 walizo zama katika bahari kutokana na chombo chao cha usafiri kuzidiwa na idadi kubwa ya watu na kuchafuka kwa habari.

Imeripotiwa kuwa zaidi ya watu 1750 wamekufa kuanzi Januari mpaka april mwaka huu wa 2015, hii ni zaidi mara 30 ya matukio yaliyo wahi kutokea.  Waanga wengi wengi husafiri umbali mrefu sana kutoka katika nchi zao mpaka kufika huko Italia.

Mhanga mmoja kutoka Gambia aitwaye Malick Touray, inasemekana mpaka kufika Italia amesafiri umbali wa kilometa 7600 sawa mailis 4750.  Mtu huyu amesafiri kwa zaidi ya mwaka 1 toka October, 2012 akiwa njiani kabla ya kufika huko Italia aliko amini kuna Maisha mazuri sana.

Kwa msaada wa taarifa kutoka shirika la habari la Uingereza (BBC), Malick alisafiri kutoka Serekunda mji uliopo Ghambia, kisha Bakamako ulioko nchini Mali, kisha Benin, Nigeria, mpaka kwenye mji wa Adege ulioko nchini Niger, kisha Qatrun, na Sabha- Tripol miji iliyoko nchini Libya. Hakika hii ni safari ndefu sana na yenye kugharimu maisha na raslimali fedha.

Malick baada ya kukaa hapo kutafuta pesa ili aweze kuingia baharini tayari kwa safari ya kwenda Italia. Alikumbanana na matukio mengi sana, ikiwemo la kufiwa na mtoto aliye zaliwa muda mfupi, maana katika ile safari ya kutoka Ghambia mpaka Libya alipata binti wakawa wapenzi, binti huyo anotoka Nigeria ambako Malick alipitia akielekea Libya. Binti yule alijifungua pale Tripoli- Libya na kwa bahati mbaya mtoto alifariki , lakini kwa kuhofia maisha yao, kwa jinsi Libya ilivyo sasa,  ilibidi wamzike mtoto kwa siri ili wasijulikane.

Safari ya kwenda Italia ilifika, lakini haikuwa rahisi, wasafirishaji wao walitaka kiasi cha Dinar 800 sawa na Euro 543 hii ni sawa na shilingi 1,145,927 kwa pesa ya Tanzania na shilingi 55,387 kwa pesa ya Kenya. Hakika ni safari ndefu yenye gharama nyingi.

Baada ya safari ndefu majini iliyokumbwa na misuko suko ya kupoteza marafiki na wasafiri wengi zaidi ya 100 walio zama majini hatimaye Malick akaifika Italia.

Je, aliyapata maisha yale mazuri aliyo yawazia na kuyatamani kwa miaka mingi? Swali ni hapana. Malick alifika Italia akaishia kuishi katika nyumba ya wakimbizi, tena ni hotel ya Don Bosco iliyo geuzwa nyumba ya muda kwa aliji ya wakimbizi. Yeye na mke wake wote hawana kazi. Ukweli ni kuwa Italia kuna maisha magumu, hakuna kazi na ni moja ya nchi za barani ulaya zilizo adhirika vibaya sana na tukio la kuanguka kwa uchumi wa dunia.



Itaendelea Kesho.

No comments:

Post a Comment