OCTOBER 06, 2013
Kwanza
kabisa natoa pole kwa wale wote waliousurika na janga la kuzama kwa boti baharini nchini
Italia katika kisiwa kiitwacho "Lampedusa", wengi wao wakitoka pembezoni kasikazini mwa
Afrika kuelekea barani Ulaya. Na Mungu azilaze roho za marehemu waliofia
baharini mahari pema peponi.
Baada ya
tukio la kuzama kwa meli nilijihisi mtu mwenye maumivu mengi moyoni na huzuni
ikinitawala juu ya vifo vya vijana wenzangu wa Afrika- tukubali kuwa tumepoteza
nguvu kazi ya Afrika!
Licha yatukio hilo kuniudhunisha, limenikumbusha matukio ya aina
hiyo kuwahi kutokea hapaTanzania. Suala
la uhamiaji ni changamoto kubwa si ulaya
tu kama vyomba vya habari vya magharibi vinavyo taarifu bali ni duniani kote, bara la
Afrikal likiwa la kwanza hususani hapa Tanzania.
Tanzania
kiujumla kuna wahamiaji wengi mithili ya walioko huko nchi za Magharibi japo tofauti ni ya kijiografia. Lakini Je ni kwanini matukio haya kutokea?
Waafrika
tumeaminishwa kuwa Ulaya ni mahali pazuri pakuishi na kazi hupatika
kiurahisi na hii ndio sababu ya kubwa ya
wimbi la wahamihaji kuongezeka kila kukicha. Matatizo ya kiuchumi
yanayo sababishwa na kuchangiwa miundo mibovu ya uduma za kijamii na serikali
dhaifu za Afrika ndio sababu nyingine inayotajwa kushindwa kutengeza au
kuzalisha ajira kwa watu wake hususani vijana na mwishowe kukimbia nchi.
Tanzania
imekuwa ikishutumiwa sana kuwa ni "njia" au "uchochoro" wa kupitisha wahamiaji haramu hasa wanaotoka
chini Eritria, Somalia na Ethiopia kwenda barani Ulaya. Tukio la Lampedusa ni
ishira ya jinsi gani matukio au suala la uhamiji linavyoanza kuwa ni "majanga".
Hapa
nchini Tanzania, Mikoa ya Tanga Arusha,
Morogoro, Iringa, mbeya ndio njia maarufu kwa wasafiri hawa haramu. Pengine ni
kwa sababu ya mfumo mbovu wa serikali yetu wa kulinda mipaka yake na haswa
suala la rushwa miongoni mwa baadhi ya maafisa wa uhamiaji.
Lakini,
cha kusikitisha zaidi ni kuwa tukio la kuzama kwa meli huko "Lampedusa"
halina tofauti na matukio ya vifo vya wahamiaji wapitiao nchini Tanzania
kuelekea nchini Afrika ya kusini kisha barani Ulaya. Lakini Je, wahamiaji hawa husafirishwa kivipi
kupitia Tanzania?
Taarifa
mbalimbali kutoka katika vyombo vya habari hapa Tanzania, vinasema wahamiaji
hawa haramu husafirishwa kwa siri kama
biashara zozote zile za magendo. Taarifa hizo uonyesha kuwa makontena makubwa yaliyozibwa na kuachwa
sehemu ndogo ya hewa , magari ya mizigo
yaendayo nchi za jirani na magari madogo hutumika kusafirishia watu hawa huku
wahamiaji hao wakitoa pesa kwa ajili ya usafiri huo.
Kwa
mujibu wa nakala ya gazeti la Tanzania Daima la nchini Tanzania la
tarehe 28,juni mwaka jana ukurasa wa
Tahariri Mwahariri anasema, nanukuu ‘’
Siri ya vifo vya raia wa Ethiopia 42 waliofariki dunia kwa kukosa hewa kwenye
roli la mizigo kwenda nchini Malawi, imejulikana. Habari ambazo gazeti hili
limezipata kutoka kwa majeruhi wa tukio hilo, zilisema kuwa walipoteza maisha
kutokana na kukosa chakula baada ya kukaa kwenye roli kwa miezi mitatu mfululizo.
Mmoja wa majeruhi 72
walionusurika, aliliambia gazeti hili kuwa tangu walipoanza hadi siku
waliyokutwa kwenye roli wilayani kongwa,Dodoma walikuwa wamemaliza miezi mitatu
wameishiwa chakula walichokihifadhi.’’
Mwisho wa kunukuu.
Ikumbukwe
pia, Machi mosi, mwaka huu, katika maeneo ya kitumbi Barabara ya Segera-chalinze,
kulitokea vifo vya Waethiopia wakiwa ndani ya makontena wakisafilishwa kutokea
Arusha kuelekea Dar es salaam. Ambapo baada ya kukamatwa baadhi walikuwa
wameisha kufa na wengine wakingali hai hizi ni kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa
mkoa wa Tanga Mh.Constantine Massawe
Mkuu wa mkoa huo alisema, wahamiaji 54 walikamatwa wakiwa kwenye makontena
yaliyokuwa yamewabeba walichanganywa na mizigi ya vitu kama vile nondo hata hivyo madereva wa magari hayo
mawili walitokomea kusikojulikana.
Lakini
swali ninalo jiuliza kwa nini nchi ya Tanzania hakuchuka hatua kama walizo
chukuwa maofisa wa serikali ya Italia?... Ndo maana nasema tukio lile la kisiwa
cha Lampedusa halina tofauti na Tanzania. Kwa Mujibu wa Waziri wa mambo ya
ndani
Swali ni Je matukio ya aina hii yataisha lini? Waafrika
tubadilike, Afrika bado ni nzuri na yenye fursa nyingi. Kukimbia matatizo
yaliyopo Afrika si sululisho la maisha yetu. Ni lazima tuyakabili kwa kupambana
na mifumo duni ya serikali zetu ili yuweze kujenga fursa za ajira.
Lakini pia tatizo hili si la Tanzania na Italia bali ni
tatizo la kila nchi hapa duniani. Ufumbuzi unahitaji nguvu ya pamoja ikiwa na
pamoja na kujenga mifumo endelevu ya ajira.
"Mwenzio akinyolewa na wewe zako tia maji".
No comments:
Post a Comment